UVCCM yafunguka kupambana
Kheri
ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na vijana wa umoja huo mjini
Dodoma na kusema lengo la kufanya hivyo ni kutokana na kuwepo na
matumaini makubwa ya kiuchumi yaliyorejeshwa na serikali ya awamu ya
tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli hivyo hawapo tayari kuona
kikundi cha watu wachache wanaotaka kuwarudisha nyuma kimaendeleo.
"kuanzia sasa endapo akiibuka mtu mwenye ujasiri wa kutukana, vijana hawatotukana bali watafanya litakaloonekana linafaa kwa maslahi ya taifa kwani wapo wanaojipambanua wazi kusifu viongozi wa ulimwengu mzima lakini kamwe hawawezi kuwapongeza na kuwasifu kwa chochote viongozi wa nchi", amesema Kheri James.
Naye Kaimu Katibu UVCCM, Shaka Hamdu Shaka amesema serikali imeona uwepo wa vijana makao makuu na kuthamani uwepo wao kutokana na kuendesha mambo kisasa zaidi.
Kwa upande wake mbunge wa viti maalum vijana, Mariam Mzuzuri amesema maamuzi na tamko la mwenyekiti wa uvccm taifa watalifanyia kazi ili vijana waweze kutambua fursa walizonazo hususania mkoani Dodoma ambako hivi sasa ni makao makuu ya nchi.

No comments: