Walimu za shule za Msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi likizo fupi kujengeana uwezo
by joina
Walimu za shule za Msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara wameamua kutumia muda wao wa likizo fupi kujengeana uwezo wa mada ngumu kwa masomo ya sayansi, Hisabati na kiingereza lengo ikiwa ni kuongeza ufanisi wa ufundishaji wa masomo hayo na hivyo kuinua ufaulu katika mitihani ya Kitaifa.
Walimu wamefikia hatua hiyo baada ya kuona baadhi ya walimu hawana uwezo wa kufundisha baadhi ya mada kutokana kutokuzielewa vizuri hivyo mafunzo hayo yatawasaidia walimu hao kuwa na uwezo wa kufundisha masomo hayo kwa ufanisi na hivyo kuongeza ufaulu wa masomo hayo.

Akiongea wakati wa mafunzo hayo katika tarafa ya Lulindi wilayani humo,
Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Ndugu Elizabeth
Mlaponi alisema kuwa mafunzo hayo ni kati mikakati ya kuongeza ufaulu
kwa matokeo ya darasa la Nne na la saba kwa mwaka 2018.
Mlaponi alisema kuwa kwa matokeo ya mwaka 2017 masomo ya Kiswahili na maarifa ya jamii ufaulu ulikuwa 50% wakati masomo ya Sayansi, Hisabati na kiingereza ufaulu ulikuwa chini ya asilimia 40 ambapo somo la kiingereza ufaulu ulikuwa chini ikifuatiwa na Hisabati

No comments: