Dogo Janja Akana Tuhuma Za Kuihofia BASATA
Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya Rap Dogo Janja
amefunguka na kuweka wazi kuwa tetesi zinazoendela kuwa yeye kuigiza
kama video queen kwenye video yake ni kwa ajili ya hofu yake dhidi ya
BASATA.
Wiki chache zilizopita Dogo Janja aliachia rasmi video yake ya wimbo wa ‘Wayu wayu’ na ilidai gumzo sana kwani ndani ya wimbo huo Dogo Janja amecheza kama video queen baada ya kujivalisha kama mwanamke jambo lililozua maneno maneno.
Sababu nyingi ziliongelewa zilizopelekea Dogo Janja kuvaa vile ikiwemo wapo waliodai alikuwa anabana bajet ya kulipa video queen lakini pia ilidaiwa aliwaogopa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) ndiyo maana akaigiza kama ‘video queen’ katika video hiyo.

Dogo Janja amekataa taarifa hizo Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers na kufunguka kuwa anashangazwa na watu kuendelea kuongelea sababu za kujifanya mwanamke katika video hiyo huku wakihusisha na Basata, alisema alichokifanya ni sehemu ya kazi za sanaa katika kufikisha ujumbe kwa jamii.Hapana, siyo kwamba niliogopa Basata, ujue hauwezi kuwa mwanasanaa kama huwezi kuichezea sanaa, nilichofanya ni ubunifu tu”.

No comments: