Wastara aibua mapya kuhusu Mange Kimambi
Msanii wa filamu nchini
Tanzania Wastara Juma amefunguka na kumchana mwanaharakati wa mitandaoni
Mange Kimambi na kusema kuwa dada huyu ana matatizo ya akili ndiyo
maana anakurupuka katika baadhi ya mambo.
"Mange Kimambi, aliwahoji madaktari India, mimi nikashangaa wale madaktari wanakuja wananiuliza kwani wewe ni nani Tanzania nikawaambia kuwa mimi ni msanii tu wa kawaida kule, wakaniuliza unamfahamu huyu mtu anajiita Mange Kimambi kwenye Instgram anasema ni dada yako, pia mwandishi wa habari anakuulizia mimi nikawaambia sina dada ana cheti cha Milembe" alisema Wastara
Mbali na hilo Wastara amesema kuwa kama Mange Kimambi angekuwa na akili timamu basi alipaswa kuangalia vizuri ile Cannula ambayo alikuwa amewekewa kwani ilikuwa imewekwa vizuri tu na wala si huo uzushi ambao yeye alikuwa anazusha.

No comments: