Askofu Masangwa Akerwa Na Manabii Wa Uongo Wanaotoza Waumini Fedha Kuwaombea
Askofu
wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya
Kaskazini Kati, Dk. Solomon Masangwa amewataka waumini wa kanisa hilo
kusimama katika imani zao wasidanganywe na manabii wa uongo wanaotoza
waumini fedha.
Aidha amewataka waumini wa kikristo nchini kuishi kwa kuzingatia imani ya dini hiyo ili kuishi maisha yanayompendeza Mungu.
Dk.
Masangwa ameyasema hayo leo Jumapili Aprili Mosi, mjini hapa alipokuwa
akihubiri katika Ibada ya Pasaka iliyofanyika katika Usharika wa Mjini
Kati Arusha na kuongeza kuwa kuna baadhi ya waumini ambao amewataka
kuacha tabia ya kutanga tanga katika dini ambapo wamekuwa wakidanganywa
na watu wanaojiita manabii na mitume.
“Kwanini
mnakubali kudanganywa, siku hizi kuna watu wanajiita manabii, mitume na
mnaenda kwao tena kwingine mnalipa kiingilio hata laki moja ili kumuona
nabii au mtume,kwanini mdanganywe na mnasahau kusimama katika imani
zenu,mnasahau ukombozi umepatikana kwa kifo na kufufuka kwa Yesu,”
amesema.
Pamoja
na mambo mengine, Askofu Masangwa amekemea vitendo vya uovu
vinavyoendelea nchini ikiwamo mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na
wizi.
“Baadhi
ya waumini wamekuwa wakitaka kuishi maisha mazuri, biashara zao kukua
kwa kasi ambapo wengine wanajihusisha na imani za kishirikina
zinazowafanya kujiingiza katika vitendo viovu.
“Kwanini
mnakwenda kukata viungo vya albino au kumrusha mwenzao au kuiba,
unakwenda kutafuta hirizi ili biashara ishamiriili maisha yawe mazuri
mnasahau Yesu ni bwana wa mabwana, Mungu ndiye anayetoa uwezo na nguvu
za kuwa tajiri, mtegemeeni si waganga,” amesema.
No comments: