Askofu Banzi: Tuwaheshimu Marehemu, Tusiwafunge Kwenye Viroba
Askofu
wa Kanisa Katoliki Jimbo la Tanga, Mhashamu Anthony Banzi ameitaka
jamii kuiheshimu miili ya marehemu kwa kuwapa maziko ya heshima badala
ya kuwafunga kwenye viroba na kuwatupa kwenye maji.
Amesema
jambo ambalo si zuri machoni kwa wanadamu na kwa Mwenyezi Mungu na pia
inakiuka utamaduni wetu kama Watanzania ambapo ameitaka jamii kubadilika
kwa vitendo vya namna kwani vinaondoa utu wao.
Ameyasema
hayo leo Jumapili Aprili Mosi, wakati akitoa salamu za Pasaka kwa
waumini wa kanisa hilo kwenye misa iliyofanyika katika Kanisa la
Mtakatifu Anthony wa Padua, Chumbageni Jijini Tanga.
“Lazima
tuwaheshimu marehemu katika nchi yetu, pengine tunataka kuwa na
utamaduni tofauti wafu wengi tunaambiwa wameokotwa ndani ya viroba
kwenye maji na kuzikwa, je hali hii inatupeleka wapi kama taifa”
Tujitafakari kwa jambo hilo.
“Kama
unavyoheshimika ukiwa mzima, marehemu pia wanapaswa kuheshimika hata
wanapokuwa wamefariki kwa kuhifadhiwa mahali ambapo hawawezi kuonekana
tena,” amesema.
Aidha,
amewataka viongozi ambao wanajukumu la kulinda usalama wa nchi,
kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani na utulivu ambayo ni tunu
tulioachiwa na waasisi wa taifa hili.
“Mara
nyingi tumesikia raia wema wametoa taarifa ya kukamatwa wahalifu hivyo
ni jukumu la waliochaguliwa kutazama usalama wao kwa lengo la
kuwawezesha kutimiza majukumu mengine ya kimaendeleo,” amesema Askofu
Banzi.
No comments: