Baada ya sare Azam waamua hivi
Taarifa
ya Azam FC leo imeeleza kuwa mapumziko hayo yameanza leo hadi jumatano
kabla ya Alhamisi kuanza tena mazoezi ya kujiandaa na mchezo ujao dhidi
ya Mtibwa Sugar.
''Mara baada ya mchezo wa jana, kikosi cha Azam FC kinatarajia kupumzika kwa siku tatu hadi Alhamisi ijayo kitakapoanza tena mazoezi kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Mtibwa Sugar utakaofanyika Uwanja wa Manungu, Turiani Morogoro Aprili 28 mwaka huu'', imeeleza taarifa hiyo.
Endapo Azam ingepata ushindi wowote kwenye mchezo wa jana ingesogea hadi nafasi ya pili na kuishusha Yanga, ambayo ingerejea katika nafasi hiyo kama ingepata matokeo mazuri kwenye mechi zake tatu za viporo.
Azam FC sasa imebaki kwenye nafasi ya tatu ikiwa na alama 47 kwenye mechi zake 26 ambazo imekwisha cheza hadi sasa. Yanga pia ina alama 47 lakini ina uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.

No comments: