Mamlaka ya hali ya hewa
iliyopo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini
Tanzania imewatahadharisha wananchi kuwepo kwa vipindi vya mvua kubwa na
upepo mkali unaozidi km 40 kwa saa katika maeneo yote ya pwani kuanzia
saa 24 zijazo kutoka sasa.
Hayo
yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na mamlaka hiyo jioni ya leo
(Jumatatu) na kudai kutakuwepo vipindi vya mvua kubwa katika saa 24
ambavyo vinatarajiwa katika maeneo ya mkoa wa Morogoro, Dar es Salaam,
Pwani, Tanga Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Mbali na hilo, TMA imesema kuna tarajiwa vipindi vifupi vya mvua
kubwa vinavyotarajiwa katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Kagera,
Mwanza, Mara, Simiyu, Kigoma, Dodoma, Singida, Kilimanjaro, Arusha na
Manyara huku upepo wa pwani unatarajiwa kuvuma kutoka kusini kwa kasi ya
km 40 kwa saa kwa Pwani yote.
Kwa taarifa kamili angalia hapa chini..
No comments: