Hakimu awa 'mbogo' kuhusu afya ya Seth
Leo
Aprili 11, 2018 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, hakimu Shaidi
amesema haipendezi kila mara amri za mahakama kutoheshimiwa na
kusisitiza kuwa chombo hicho cha dola kinafanya kazi kwa mujibu wa
sheria.
Hakimu Shaidi ametoa kauli hiyo baada ya
wakili wa Serikali, Nassoro Katuga kueleza agizo lililotolewa na
mahakama la kumpeleka Seth Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa
matibabu halijatekelezwa na kwamba wanasubiri taarifa kutoka kwa
mshtakiwa kuhusu daktari wake na kwamba sababu nyingine iliyowafanya
washindwe kutekeleza agizo la mahakama kwa wakati ni mshtakiwa
kuhamishwa kutoka gereza la Segerea kwenda gereza la Ukonga.
Hata hivyo Wakili wa utetezi, Hajra
Mungula amepingaana na utetezi wa aakili Katuga na kudai kuwa mshtakiwa
hajaongea chochote na kwamba wanashtushwa na maneno yaliyotolewa na
upande wa mashtaka.
Mungula amedai kuwa agizo la mahakama
wakati linatolewa Machi 28, 2018 tayari mshtakiwa huyo alikuwa
amekwishapelekwa gereza la Ukonga na kuongeza kwamba hali ya Seth si
nzuri na kwamba suala la afya si la mzaha “hatuwezi kuendelea na kesi
mtu akiwa mgonjwa.”
Pamoja na hayo Wakili huyo amedai kuwa
imekuwa ngumu kwenda kumuona gerezani Bw. Seth na hata kumpa dawa na
kwamba hawajui upande wa mashtaka unadhamira gani huku akisisitiza kuwa
haruhusiwi mtu yeyote kumuona hata mke wake wa ndoa na kuomba mahakama
iliangalie hilo.
Seth na Rugemalira wanakabiliwa na
mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na kuisababishia
Serikali hasara ya Dola za kimarekani 22, 198,544.60 (Sh309.5bilioni)
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Hakimu Shaidi ameahitisha kesi hiyo mpaka April 25 kwa ajili ya kutajwa.

No comments: