Jeshi la Polisi litawajibika – CHADEMA
Kauli
hiyo imetolewa na CHADEMA kupitia taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya
habari na Mkurugenzi wa Itifaki na Mawasiliano ya Mambo ya Nje, John
Mrema, na kueleza kuwa iwapo afya ya Halima Mdee ambaye ametoka
kufanyiwa upasuaji nchini Afrika Kusini, ikitetereka kwa namna yoyote
ile, basi itawajibika juu ya hilo.
Sambamba na hilo CHADEMA wametoa wito wa kumpatia dhamana mbunge huyo, ambaye mpaka sasa anashikiliwa na jeshi la polisi katika kituo cha kati jijini Dar es salaam.
"Tunasikitishwa na kulaani kitendo hiki cha polisi kuendelea kumshikilia mgonjwa ambaye alikuwa amelazwa hospitalini. Jeshi la Polisi litawajibika kwa watanzania endapo afya ya Mhe. Halima Mdee ikitetereka au ikidhoofu zaidi na lawama zote. Tunatoa mwito kwa Jeshi la Polisi limpatie dhamana ili aweze kuendelea na matibabu yake, kwani dhamana ni haki yake na zaidi ni kuwa huyu bado ni mtuhumiwa na ni Mgonjwa ambaye ametoka hospitalini", imesema Taarifa hiyo.
Halima Mdee alikamatwa leo asubuhi katika uwanja wa ndege wa Mwl. Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Afrika Kusini, alikokuwa akipatiwa matibabu.

No comments: