Yanga yakalishwa na Singida United
Katika
dakika 45 za kipindi cha kwanza katika mchezo huo timu ya Yanga
ilifanikiwa kupata bao lake la kwanza kupitia mchezaji wake Yusuf Mhilu
kwa kutumia mpira wa kichwa akiunganisha kona ya Ibrahim Ajib Kayika
kwenye dakika ya 23 ya kipindi cha kwanza cha mchezo na kupelekea timu
yake kuongoza kipindi chote cha kwanza mpaka kuisha licha Singida United
kuonesha jitihada za kutaka kusawazisha bao hilo lakini kwa bahati
mbaya juhudi zao hazikuweza kuzaaa matunda.
Dakika 45 za pili za mchezo huo, Singida
United walifanikiwa kusawazilisha bao la wapinzani wao kupitia mchezaji
wao Kenny Ally na mpaka kipinga cha mwisho kinapulizwa timu hizo
zilitoka sare ya kufungana mabao 1-1 na kusababisha kupigwa mikwaju ya
matuta na kuifanya Singida United kutoka kifua mbele baada ya kupata
mikwaju 4-2 dhidi ya wapinzani wao Yanga SC.
Kutokana na ushindi huo, timu ya Singida
United imejikatia tiketi ya moja kwa moja ya kuchuana na JKT Tanzania
katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho.
Timu ya Yanga kwa sasa itakuwa imebakia
na taji moja mkononi inalowania katika msimu huu wa mwaka 2018/2019
baada ya kutolewa leo katika michuano ya kombe la Shirikisho na Singida
United kwenye dimba la Namfua mkoani Singida.
No comments: