Makonda asisitiza kuweka mgomo
Akizungumza
leo na wananchi waliojitokeza katika ofisi yake kutafuta msaada wa
kisheria baada ya kutelekezewa watoto na wenzi wao, Makonda amesema
hatakuwa tayari wala kuwa na muda wa kumsikiliza mwanaume
aliyemtelekeza mwanamke na mtoto na kwamba kwa sasa yupo kusaidia wapate
haki zao.
Aidha amesema kwamba kati ya wazazi waliofika ofisini kwake amegundua wapo watu wa makundi tofauti tofauti waliofika ofisini kwake ambapo kundi la kwanza ameshukuru na analipongeza kwa kuwa wameamua kumaliza tofauti zao baada ya kusikia mambo yamefika kwake.
Mbali na hayo Makonda amesema wale watu wanaolalamika mitandaoni kwa kudai kuwa kulitakiwa kufanyike kwa usiri wa jambo hilo, wanapaswa kutoa huduma kwa watoto wao ili wasiabishwe hadharani.
Aidha ameweka wazi kwamba mpaka sasa mezani kwake yapo majina ya watu mashuhuri 107 ambao nao wametajwa kutelekeza watoto wao.

No comments: