Makonda 'Awashitaki' Kwa Rais Magufuli Wanaoingia Dar na Kutoa Matamko ya Kichochezi
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam amewashtaki kwa Rais Magufuli baadhi ya watu
(hajawataja kwa majina) kwa kudai kuwa wanaingia ndani ya mkoa wa Dar es
salaam na kutangaza uchochezi.
Mh.
Makonda amewasilisha mashtaka hayo kwa Rais leo wakati alipokuwa
akiweka jiwe la msingi la ujenzi mradi wa kuongozea ndege katika vituo
vinne hapa nchini.
Mh.
Makonda amemuambia Rais Magufuli kwamba kuna watu wanaingia ndani ya
mkoa wa Dar es salaam na kutangaza uchochezi hivyo yeye kama kiongozi wa
mkoa wanajaribu kuangalia utaratibu mzuri wa kisheria watolee matamko
katika mikoa yao.
Aidha amesema kwamba
"Mh. Rais Tumesikia sikia huko kwingine ila sisi kwetu hakuna waraka.
Hakuna waraka popote pale ulipopita. Watu wamemwabudu bwana na mwokozi
wao na Tumeungama dhambi zetu kupitia kufa kwake msalabani, tumefufuka
naye na tunaendelea kufanya kazi kikamilifu".
Mbali
na hayo Mku huyo wa Mkoa ameweka wazi kwamba wakazi wa Mkoa wa Dar es
salaam wamesherehekea sikukuu ya Pasaka salama salimini kwani wananchi
wametambua thamani ya amani.
No comments: