Mbunge Alalamikwa Kupapaswa Sehemu Nyeti na Walinzi wa Bunge
Mbunge
wa Kavuu, Dk. Pudenciana Kikwembe (CCM), amedai kuwa walinzi
wanaowakagua wakati wakiingia kwenye viwanja vya Bunge, wanawapapasa
sehemu mbalimbali za miili yao.
Mbunge
huyo amesema hayo leo wakati akiomba mwongozo wa kiti, jambo
lililofanya Spika wa Bunge, Job Ndugai, kupiga marufuku ukaguzi wa aina
hiyo.
Amesema
wanapopita kwenye mashine za ukaguzi hutakiwa kuvua mikanda, viatu, saa
na vitu vingine na kwamba kibaya zaidi kwake ni suala la kupapaswa.
“Tunavua
nguo, watu wanainua mashati kuvua mikanda na tunaona vitovu vya wanaume
halafu miili inasisimka tukidhani wanataka kufanya maandalizi ya, mwili
wa binadamu una vivutio vingi.
“Leo
nimepita mashine moja vizuri na nilipofika ya pili ikalia. Nikaambiwa
nikaguliwe sasa kibaya nakwenda kukaguliwa ananishikashika maeneo
mbalimbali, hapa tuna mwezi mmoja huku si kutiana hanjamu,” amehoji.
Dk. Kikwembe amemtaka Spika kutoa agizo kukomesha jambo hilo, akisema halikubaliki na linawadhalilisha wabunge kila wakati.
Akijibu
mwongozo huo, Spika wa Bunge, Job Ndugai ameagiza ukaguzi kwa kuwashika
shika wabunge mwilini uachwe mara moja kwa kuwa unawadhalilisha na
kuagiza utaratibu ufanyike kwa kuangalia namna bora ya kuwakagua wabunge
kwani kinachofanyika ni ukaguzi wa kizamani uliopitwa na wakati.

No comments: