Mtama, Ndizi, Mihogo Vyachangia Kushuka Kwa Mfumuko Wa Bei
Mfumuko
wa bei wa taifa kwa mwezi Machi, umepungua hadi kufikia asilimia 3.9
ikilinganishwa na asilimia 4.1 ilivyokuwa Februari, mwaka huu.
Baadhi
ya bidhaa za vyakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei ni mtama
kwa asilimia 7.1, unga wa muhogo asilimia 6.7, maharagwe asilimia 3.9,
mihogo mibichi asilimia 16.6 na ndizi asilimia 16.7.
Mkurugenzi
wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS),
Ephraim Kwesigabo amesema hayo leo alipozungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam.
Amesema
hali hiyo inamaanisha kwamba kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na
huduma kwa mwaka ulioishia Machi imepungua ikilinganishwa na kasi
ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia Februari.
“Hali
ya mfumuko wa bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki, nchini Uganda
umepungua hadi asilimia 2.0 Machi, kutoka asilimia 2.1 Februari, mwaka
huu huku Kenya ukipungua hadi asilimia 4.18 Machi, kutoka asilimia 4.46,
Februari, mwaka huu,” amesema.

No comments: