Mke wa zamani wa Nelson Mandela Afariki Dunia
Winnie
Mandela, mke wa zamani wa Nelson Mandela, ambaye pia alipigana dhidi ya
utawala wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini amefariki dunia akiwa na
miaka 81. Habari za kifo chake zimethibitishwa na msaidizi wake.
Winnie
alizaliwa mnamo 26 Oktoba mwaka 1936, na ingawa yeye na mumewe - Nelson
Mandela - walitalikiana mapema miaka ya 1990, Winnie Madikizela Mandela
kama alivyofahamika rasmi alisalia kutoa mchango katika maisha ya Bw
Mandela.
Msemaji
wa familia Victor Dlamini amesema kupitia taarifa kuwa: "Amefariki
baada ya kuugua kwa muda mrefu, ambapo amekuwa akiingia na kutoka
hospitalini mara kwa mara tangu mwanzo wa mwaka.
"Alifariki mapema Jumatatu adhuhuri akiwa amezungukwa na familia na wapendwa wake."
Askofu
mstaafu na mshindi wa tuzo ya Nobel Desmond Tutu amemsifu kama "ishara
kuu ya vita dhidi ya ubaguzi wa rangi," kwa mujibu wa AFP.
Winnie alikuwa na miaka 20 hivi pale alipojipata katika siasa.
Alisomea kazi ya utoaji huduma za kijamii na haraka aliyazoea maisha ya kuwa mama na mwanasiasa.
Katika
kipindi chote cha miaka 27 mumewe alipokuwa gerezani bila matumaini ya
kuachiwa huru kutokana na hukumu ya kifungo cha maisha jela alichopewa
mwaka 1964, Bi Winnie alilazimika kubeba jukumu la ulezi wa watoto na
pia kuendeleza kampeni za kisiasa kutaka mashujaa wa kupigania nchi yao
waachiwe huru hasa mumewe.
"Kamwe
hatutapoteza matumaini na watu wangu hawatapoteza matumaini kamwe, bila
shaka tunatarajia kwamba kazi itaendelea," alisema wakati huo.
Kutokana
na hayo Bi Winnie Mandela alilazimishwa kusalia tu huko Brandford
katika jimbo lao la Orange Free katika miaka ya 70 baada ya operesheni
mojawapo za kupambana na ubaguzi wa rangi zilizokuja kujulikana zaidi
kama the Soweto Uprising.
Bi Mandela (pichani mwaka 1988) alihusika makubwa kukabiliana na utawala wa ubaguzi wa rangi Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bi Mandela (pichani mwaka 1988) alihusika makubwa kukabiliana na utawala wa ubaguzi wa rangi
Kama
ilivyomtokea mumewe, Bi Winnie alifungwa gerezani, na hata kuwekwa
katika kizuizi cha pekee yake ambacho ni mojawapo ya vifungo vigumu
zaidi gerezani vinavyowaathiri wafungwa kisaikolojia.
Lakini
baada ya kuachiwa kwake mtindo wa mapambano yake dhidi ya ubaguzi wa
rangi ulianza kupata sifa mbaya hasa pale alipoonekana kuendekeza tabia
ya kuwavisha tairi shingoni wale waliolengwa kwa tuhuma za usaliti na
kisha kuwachoma moto.
"Kwa 'mikufu yetu' tutaikomboa nchi hii," alizoea kusema.
Mambo
yalizidi kumwendea mrama kutokana na matendo ya baadhi ya walinzi wake
katika kile kikundi kilijulikana kama the Mandela United Football Club.
Walipatikana
kuhusika katika kitendo cha kumteka nyara na kumuua kijana mmoja mwenye
umri wa miaka 14 aitwae Stompie Moeketsi -kwa tuhuma za kwamba alikuwa
akitoa siri kwa maadui zao.
Japo
Bi Winnie Mandela aliepuka hukumu ya kifungo jela - baadaye tume ya
ukweli na maridhiano iliyoongozwa na askofu Desmond Tutu, iliyokuwa
inachunguza ukweli kuhusu matendo tata katika vita dhidi ya ubaguzi wa
rangi na kutafuta maridhiano, ilimpata Bi Mandela na hatia ya
kutowajibika kisiasa wala kimaadili wakati wa kitendo hicho.
ANC
leader Nelson Mandela and wife Winnie raise fists upon his release from
Victor Verster prison, 11 February 1990 in Paarl Haki miliki ya picha
AFP
Image caption Nelson na Winnie Mandela baada yake kuachiliwa huru Februari 1990
Licha
ya misukosuko hiyo Bi Mandela alibaki kuwa mtu muhimu sana katika siasa
za Afrika kusini na kuwa mwakilishi muhimu waa wanawake waliopambana
kufa na kupona dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi uliokuwa
unaendelezwa na Wazungu walio wachache nchini humo.
Katika
siku za baada ya uhuru wa Afrika Kusini anakumbukwa zaidi kwa kuwa
miongoni mwa wachache katika uongozi wa ANC waliomuunga mkono aliyekuwa
rais wa Afrika Kusini Thabo mbeki katika kushtumu na kulaani vikali
vitendo vya kuwashambulia wahamiaji wa Kiafrika huko nchini Afrika
Kusini.
KUSINI
- mashambulio yaliyobadikwa jina xenophobic attack. Pia amekuwa
muungaji mkono mkubwa wa kiongozi wa chama cha Economic Freedom Fighters
CHA Julius Malema , kilichojimegua kutoka ANC ambacho kilimkosoa vikali
rais aliyelazimika kung'atuka Jacob Zuma.
Historia
ya Bi Winnie Madikizela Mandela, hadi kifo chake inabaki akikumbukwa
zaidi kama mama wa taifa la Afrika kusini aliyesimama kidete dhidi ya
ubaguzi wa rangi katika umri wake wote.
No comments: