Mvua yauwa wawili Mwanza na kujeruhi
Wakati mvua zikiwa
zinaendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi na kusababisha
mafuriko, huko Jijini Mwanza watoto wawili wa familia moja wamefariki
baada ya kudondokewa na ukuta kipindi mvua hizo zikinyesha zilizokuwa na
upepo mkali.
Akizungumza
kutoka kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Ahmed Msangi
amesema watoto hao wamefariki majira ya usiku wakati wakiwa wamelala
katika nyumba waliyokuwa wanaishi katika mtaa wa Buguku kata ya Buhongwa
wilayani Nyamagana Jijini Mwanza.
Kamanda Msangi amewataja watoto hao kuwa ni Mariam Saimon (4) pamoja na Musa Baraka (2) hukyu majeruhi wakiwa watatu katika tukio hilo.
Msikilize hapa chini Kamanda Msangi akielezea zaidi undani wa tukio hilo.

No comments: