Mwigulu ataka wakamatwe na wasiachiliwe
Mwigulu
ametoa kauli hiyo leo (Aprili 05, 2018) katika Mkutano wa 11 wa kikao
cha Bunge cha tatu kilichofanyika katika mkoa wa Dodoma wakati akitoa
taarifa ya ajali iliyotokea wilayani igunga jana kwa kuhusisha lori aina
ya fuso na basi la abiria la kampuni ya city boys na kuua watu 12.
"Taarifa za awali tulizopewa
kwamba chanzo cha ya ajali hiyo sio mashimo ya barabarani pekee yake
bali ni mwendo kasi wa dereva wa fuso ambaye alisababisha kuligonga basi
hilo hivyo naliagiza jeshi la polisi popote pale watakapomkamata dereva
anatembea mwendokasi pamoja na hiyo ya kutoza faini, wamuweke ndani
wasimuachie mpaka pale watakapompeleka Mahakamani ili hatua zaidi ziweze
kuchukuliwa", amesema Mwigulu.
Pamoja na hayo, Mwigulu ameendelea kwa kusema "endapo
dereva huyo akitoka Mahakamani na kama rekodi zake ni mwendokasi basi
anyang'anywe leseni yake ili asiweze kuendelea kuendesha magari
yanayosababisha ajali na kupoteza maisha ya watu kama hivi jana
ilivyotokea".
Kwa upande mwingine, Rais Magufuli
amewataka viongozi wote wanaohusika na usimamizi wa usalama wa
barabarani kutafakari kwa nini ajali nyingi zimekuwa zikitokea katika
maeneo yaleyale na kutafuta ufumbuzi ili kuepusha madhara ya watu
kupoteza maisha, kupata ulemavu wa kudumu na kupoteza mali.

No comments: