Kesi ya Aveva na Kaburu aunganishwa mwingine
Kesi inayowakabili viongozi
wa juu wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na Geofrey Nyange 'Kaburu'
imeharishwa kwa mara nyingi tena leo hadi Aprili 12, 2018 kufuatilia
ombi la upande wa mashtaka kudai wanataka kumuongeza mshtakiwa mmoja
katika kesi hiyo.
Hayo
yameelezwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es
Salaam Thomas Simba, na Wakili wa Serikali kutoka TAKUKURU, Leornad Swai
na kusema kesi hiyo ilifikishwa Mahakamani hapo kwa ajili ya washtakiwa
kusomewa maelezo ya awali baada ya upelelezi wa kesi yao kukamilika.
Hata hivyo, Wakili Swai aliiomba
Mahakama ahirisho fupi kwa kuwa wanatarajia kufanyia mabadiliko katika
hati ya mashtaka kwa kuongeza mshtakiwa mmoja.
Kufuatia ombi hilo, Mahakama iliamua
kuahirisha kesi hiyo hadi Aprili 12 mwaka 2018 kwa ajili ya upande wa
mashtaka kufanya mabadiliko yao na washtakiwa kusomewa maelezo ya awali.
Aveva na Kaburu kwa pamoja walipandishwa
Mahakamani kwa mara ya kwanza Juni 27 mwaka 2017 wakiwa wana kabiliwa
na mashtaka ya uhujumu uchumi ikiwemo ya kughushi, kuwasilisha nyaraka
ya uongo na utakatishaji wa fedha.

No comments: