Nyota wa Singida arejea kwaajili ya Yanga
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi wa timu hiyo Festo Sanga, nyota huyo aliondoka
nchini na kurejea kwao nchini Rwanda kwa ruhusa maalum ya klabu kwa kile
kilichoelezwa ni kwenda kushughulikia matatizo ya kifamilia.
''Tayari Dany amewasili Dar es salaam tangu jana jioni na ameungana na timu ambayo ipo jijini hapa ikifanya maandalizi ya mwisho kwaajili ya mchezo wetu muhimu kesho dhidi ya Yanga'', amesema Sanga.

Singida United inayoshika nafasi ya tano kesho itacheza mchezo wake wa marudiano kwenye ligi kuu na Yanga inayoshika nafasi ya pili kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam. Katika mchezo wa raundi ya kwanza timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
Mchezo wa mwisho timu hizo kukutana ilikuwa ni wiki moja iliyopita ambapo ulikuwa ni mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya robo fainali na Singida United ilishinda kwa penalti 4-2 baada ya kutoka sare ya 1-1 katika dakika 90.

No comments: