Werrason kufanya kazi na Christian Bella
"Imethibitishwa sasa nitafanya kazi na Werrason the king of jungle, nadhani kujituma juhudi zangu na kutokata tamaa leo hii ma Star Wakubwa ambao nilikua nawashangaa kwenye TV nikiwa mdogo kutoka DRC wananipa heshima na kunikubali. Nasema Asante Mungu Asante pia sana Kwa watanzania kwa kunipa na fasi na kunikubali na kuni support leo hii miaka 13 kwenye game bado naonekana mpya" alisema Christian Bella
Christian Bella kwa sasa anatamba na wimbo wake 'Niende wapi' ambao amemshirikisha rapa Joh Makini kutoka katika kampuni ya Weusi. Itazame hapa kazi yake mpya.

No comments: