Rais Magufuli kuhutubia Bunge la Bunge la Afrika Mashariki(Eala) Dodoma
Rais
John Magufuli anatarajiwa kulihutubia Bunge la Afrika Mashariki(Eala)
katika mkutano wake wa nne kikao cha kwanza ulioanza leo mjini Dodoma
ikiwa ni mara ya kwanza vikao vya bunge hilo kufanyika huko.
Taarifa
ya Eala kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Ofisa Habari Mwandamizi,
Bobi Odiko ilisema mkutano huo utafanyika kati April 9 hadi 28 mwaka huu
na Rais Magufuli atalihutubia katika muda utakaopangwa na taarifa
itatolewa wiki ijayo.
Spika
wa Bunge hilo, Martin Ngoga ataongoza mkutano huo wa wiki tatu ambao
utajadili miswada na maazimio mbalimbali wakati kamati za bunge
zimeendelea kuandaa miswada kwa ajili ya mkutano huo.
“Kwasasa
ipo miswada miwili itakayojadiliwa kwa kina inayohusu Itifaki ya Sarafu
Moja ambayo ni mswada wa taasisi ya Fedha na mswada wa Takwimu yote ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki ya mwaka 2017,”alisema Odiko.
Amesema
miswada hiyo iliwasilishwa katika bunge hilo na Mwenyekiti wa Baraza la
Mawaziri wa EAC, Dk Kirunda Kivenjija na ilishasomwa kwa mara ya
kwanza katika mkutano wa pili uliofanyika Januari jijini Kampala.
Taarifa
imesema lengo la mswada wa taasisi ya Fedha ya EAC wa mwaka 2017
unakusudia kuanzisha taasisi ya jumuiya ambayo itakua na majukumu ya
kuweka taratibu za kuanza Umoja wa Sarafu wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki.
“Kwa
mujibu wa Ibara ya 23 ya Itifaki iliyoanzisha Jumuiya ya Afrika
Mashariki inataja Umoja wa Sarafu ya EAC, hivyo muswada huo unatarajiwa
kuweka majukumu, uongozi na namna ya kupata fedha za kuendesha taasisi
hiyo,”alisema Odiko.
Pia
muswada wa Takwimu wa EAC wa mwaka 2017 unalenga kuanzisha taasisi ya
takwimu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kama inavyotajwa kwenye Mkataba
wa EAC ibara ya 9 na 21 ya Itifaki iliyoanzisha Umoja wa Sarafu wa
EAC.
Amesema
Baraza la Mawaziri wa EAC wanatarajiwa kukutana mapema na kamati
mbalimbali za bunge hilo kupitia mambo muhimu ya miswada hiyo huku
kamati ya Mawasiliano, Biashara na Uwekezaji ikitarajiwa kukutana na
wadau juu ya muswada wa Takwimu wa EAC.

No comments: