Msigwa Adai Wafungwa Segerea Wanalala Kwa ‘Alarm’
Mbunge
wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema), amedai Tanzania kwa
sasa kuna msongamano mkubwa wa wafungwa na mahabusu magerezani hususani
Gereza la Segerea.
Amesema
kutokana na hali hiyo, wafungwa na mahabusu wa gereza hilo wanalazimika
kulala upande mmoja mmoja kwa zamu baada ya muda inapigwa ‘alarm’ kisha
wanageukia upande mwingine hatua aliyosema ni ukiukwaji wa haki za
binadamu na watoto.
Akiuliza
swali la nyongeza leo bungeni Msigwa amesema Gereza la Segerea
limezidiwa na mahabausu ambapo lina uwezo wa kuchukua mahabusu 700,
lakini waliopo sasa ni mahabusu na wafungwa 2,400.
“Ukienda
katika magereza zetu kuna msongamano mkubwa sana kwa mfano Gereza la
Segerea ambalo nililipitia juzi lina uwezo wa kuchukua mahabusu 700
lakini sasa hivi lina mahabusu na wafungwa 2,400.
“Ni
kwanini Serikali imekuwa ikipeleka wanasheria wao ambao wamekuwa
wakilazimisha wale ambao wanaweza kupata dhamana waende kukaa mahabusu
kama ambavyo kesi zetu zilikuwa zina dhamana lakini mawakili wa Serikali
walikuwa wanalazimisha tuende kule tukaongeze msongamano,” amehoji
Msigwa.
Akijibu
kwa niaba ya Serikali, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,
William Ole Nasha amesema kuwekwa ndani kwa muda mrefu kwa mahabusu si
kweli kwamba Serikali haitaki kesi hizo zimalizike haraka.
“Sababu
za msingi ni sababu ya usalama wao, wakienda nje wanaweza wakapata
matatizo ikiwamo Serikali kuwalinda pili kuna watuhumiwa wakitoka nje
wataenda kuharibu ushahidi,” amesema.

No comments: