Serikali imesema,
imefanikisha kuyashughulikia matukio 1,072 kwa mwaka 2017
yaliyoripitiwa kupita namba maalum iliyotolewa na Serikali kwa ajili ya
kuripoti matukio ya udhalilishaji na unyanyasi hususan Wanawake na
Watoto.
Akizungumza
leo Bungeni Mjini Dodoma, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile, amesema hiyo ni kati ya
mikakati mingi iliyowekwa na serikali kwa ajili ya kukomesha matukio ya
udhalilishaji kwa watoto nchini.
Aidha, Dk. Ndungulile amesema, Wizara yake tayari imeshatoa mafunzo
kwa Maafisaa Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii wapatao 50 katika
mikoa yote 26 kwa ajili ya kuanzisha Kamati za Ulinzi kuanzia ngazi ya
kijiji hadi Taifa ili kupunguza kama si kumaliza kabisa tatizo hilo.
No comments: