Mbunge atoa siri ya kuua upinzani
Mh. Mtolea ameweka wazi hayo wakati akizungumza na www.eatv.tvambapo
amesema iwapo wananchi watapatiwa yale ya msingi vyama vinavyoitwa vya
upinzani vinaweza kukosa hoja ya kukosoa lakini siyo kuviua kabisa kwani
hata huko Marekani ambapo wameshapigana kwa kiasi kikubwa na maadui
watatu bado kuna vyama vingi kwa ajili ya kurekebishana.
Aidha Mbunge huyo ambaye yupo chini ya Mwamvuli wa UKAWA amesema kwamba licha ya Tanzania kwa sasa kutokuwa na uwanja mzuri wa kufanyia siasa lakini anaamini kwa watu wanaoamini siasa za upinzani hata wakipewa nusu saa ya kufanya kazi hiyo itawatosha kabisa kwani ambacho wanachokizungumza kipo ndani ya jamii.
Ameongeza kwamba kuwa hatamani kusikia hata siku moja kwamba vyama vya upinzani nchini vitakufa kwani watu kama yeye bado wapo wanaoamini ndani ya upinzani .
"Sitamani kusikia kwamba vyama vya upinzani vinakufa. Bado tupo sisi tunaoamini ndani ya upinzani na nina uhakika hata tukiachiwa nusu saa ya kuzungumza tutafanya tuu kwani yale tunayozungumza hayatoki hewani. Hata tukifunguliwa 2020 tukaambiwa fanyeni siasa itatosha maana siasa ni maisha ya kila siku ya mwananchi. Ukitaka kutuua tekeleza yale wanayoyataka kwani sisi tukiongea tunaonyesha yale makosa"- Mtolea

No comments: