Serikali yamtambua Roma Mkatoliki
Roma
Mkatoliki leo April 5, 2018 amekwenda Baraza la Sanaa la Taifa na
kujisajili kama ambavyo aliagizwa na viongozi wa serikali na kusema
kuanzia leo atakuwa huru kufanya kazi na sasa anarudi rasmi katika
muziki.
Mar 1, 2018 Msanii wa muziki wa Hip Hop bongo Roma Mkatoliki alifungiwa kufanya shughuli za muziki kwa muda wa miezi sita kwa kile kilichodaiwa msanii huyo kudharua wito wa BASATA na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Msanii huyo ametumikia kifungo hicho kwa mwezi mmoja na siku tano hivyo kifungo chake kimeisha leo baada ya kujisajili BASATA.
Msanii Roma Mkatoliki ajisajili na kukabidhiwa rasmi cheti cha kutambulika na Baraza la sanaa la Taifa leo April 05 2018, Hii ni baada ya kupewa sharti na Wizara ya Habari ya kujisajili kwanza Basata ili aondolewe adhabu yake ya kufungiwa miezi 6.

No comments: