Toka Twitter: Ushauri wa Waziri January Makamba kwa wasanii na vijana maarufu
Ujumbe
huu umeandikwa leo na Waziri January Makamba katika ukurasa wake wa
Twitter ikiwa ni ushauri kwa wasanii na vijana maarufu.
Ushauri
huu umechukuliwa na wengi wa watumiaji wa mitandao ya Twitter na
Instagram kama muhimu kwa wasanii hasa baada ya kuibuka kwa matendo
yasiyoakisi taswira njema kwa jamii kwa siku za karibuni.
Ujumbe huo umeandikwa kwa lugha ya Kiingereza lakini tafsiri isiyo rasmi ni:
“Kwa
wadogo zangu maarufu wa kike na wa kiume: umaarufu unabeba majukumu.
Ushike kwa makini. Umaarufu unaweza kudumu kwa dakika 15 watu tukafurahi
na kukuona muhimu – kisha maisha yakaendelea. Umaarufu pia unaweza
kudumu milele, ukafa kimwili lakini jina lako lisife. Umaarufu pia
unaweza kudumu na kufikia kiwango cha kukuharibu na kukuondoa kwenye
mstari.”
Mmojawapo ya wasanii waliojibu ujumbe huo Twitter ni Vanessa Mdee ambaye ameshukuru


No comments: