Tume ya Uchaguzi yapata pigo....Watatu Wajiuzulu kwa Mpigo
Tume
huru ya Uchaguzi nchini Kenya IEBC imepata pigo kubwa baada ya
watumishi wake watatu kuacha kazi kwa mpigo, huku wakilaumu uongozi wa
Tume hiyo
Wafanyakazi
hao ambao ni Kaimu Mwenyekiti Consolata Nkatha Maina, Kamishna Margaret
Mwachanya na Paul Kurgat wamejiuzulu wadhifa wao na nafasi zao za kazi
ndani ya tume hiyo, huku wakisema kwamba Mwenyekiti wa IEBC Wafula
Chebukati ameshindwa kuongoza.
“Kwa
muda mrefu sana na mara nyingi mno, mwenyekiti wa tume ameshindwa kuwa
na mkono thabiti na imara, badala yake chini ya uongozi wa Chebukati,
bodi ya tume imekuwa mahali pa kutembea kwa habari zisizo za ukweli,
misingi ya kutokuaminiana na kujitafutia sifa binafsi.
"Taasisi imesababishwa kutoweza kufanya uamuzi, kuvuja nyaraka za ndani ili kutumikia malengo binafsi na kufuata maslahi binafsi, yote ambayo ni kinyume na sheria iliyowekwa ambayo inasimamia mwenendo wa uongozi wa tume na wafanyakazi”, wamesema wafanyakazi hao ambao miongoni mwao yumo Kaimu Mwenyekiti wa Tume.

Hivi
karibuni Mwenyekiti wa Tume hiyo Wafula Chebukati amempa likizo ya
lazima Mkurugenzi wa Tume Ezra Chiloba bila sababu maalum, huku wengi
wakilaumu kitendo hicho, wakisema kuwa Chebukati anaendesha Tume kwa
maslahi yake binafsi.
IEBC
imekuwa ikilaumiwa kwa matukeo ya uchaguzi wa mwaka 2017 wa viongozi wa
Kenya, ambao pia ulisababisha kufutwa kwa matokeo ya Urais, kwa
uchaguzi wa Agosti 8, 2017.

No comments: