Header Ads

Waziri Mkuu atoa tamko kwa viongozi wa dini




Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaomba viongozi wa dini popote walipo wahakikishe wanaipigania na kuilinda amani kwa kila hali ikiwa ni pamoja na kupambana na viashiria vya uvunjifu wa amani.
Waziri Majaliwa ametoa kauli hiyo kwenye Mkutano Mkuu wa BAKWATA uliofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma, ambapo amesisitiza kuwa ni muhimu wasaidizi wa Mufti wakasimamia suala hilo.
"Dini ni taasisi muhimu sana kwa maisha yetu ya kila siku ndio maana serikali inaheshimu na kuzitambua dini zote kutokana na mchango wake mkubwa katika amani ya nchi yetu. Niwaombe viongozi wangu popote mlipo muilinde amani yetu", amesema Waziri Majaliwa.
Waziri Mkuu amesema amani ni miongoni mwa neema kubwa kwa binadamu na ndiyo maana wote wanamtambua Mwenyezi Mungu, hivyo wasiruhusu mtu au kikundi chochote kujaribu kuchafua na kuharibu amani iliyopo nchini.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewasisitiza viongozi Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) wahakikishe kuwa chombo hicho kinaendelea kuwaunganisha waislamu bila ya kujali makabila yao, rangi zao au madhehebu yao. 
Waziri Mkuu amesema Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakar bin Zubeiry ambaye ndiye kiongozi wa Waislamu nchini mara zote amekuwa akisisitiza jambo hilo na kuwataka waislamu popote walipo watambue kuwa hicho ni chombo chao

No comments:

Powered by Blogger.