Zidane awapangua Ronaldo na Bale
Kiungo Luka Modric pia ameondolewa kwenye kikosi cha wachezaji 20 hivyo kufanya timu hiyo kusafiri kwenda La Rosaleda na wachezaji 19 pekee. Inaaminika nyota hao watatu wameachwa ili kuwapa nafasi ya kuwa vizuri kwenye mechi dhidi ya Bayern Munich.
Real Madrid ambayo inashika nafasi ya 4 leo inaweza kurejea katika nafasi ya 3 endapo itaibuka na ushindi huku Malaga inapigania kukwepa kushuka daraja ikiwa inaburuza mkia.

No comments: