Header Ads

Bocco na Okwi wakalishwa na nyota wa Majimaji



Mshambuliaji wa timu ya Majimaji ya Songea yenye maskani yake Mkoani Ruvuma, Marchel Kaheza amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa ligi kuu soka Tanzania Bara (VPL) kwa mwezi Aprili.
Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) alasiri ya leo Aprili 13, 2018 na kusema Kaheza ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda

wachezaji wenzake wawili ambao ni John Bocco pamoja na Emmanuel Okwi wote kutokea timu ya Simba SC.
TFF imesema maamuzi hayo yamefikiwa baada ya kufanyika uchambuzi ndani ya wikii hii na Kamati ya Tuzo iliyochaguliwa na shirikisho na hatimaye kumpata mshindi.
Kaheza aliisaidia Majimaji kwa kufunga mabao 7 kwa mwezi wa Aprili ambapo kati ya mabao hayo matatu amepiga 'hat trick' kwenye mchezo mmoja.
Mwezi Aprili Majimaji ilicheza michezo minne na kupata pointi 7 baada ya kushinda michezo miwili, sare mmoja na kupoteza mchezo mmoja na kusababisha kupanda kutoka nafasi ya mwisho iliyokuwepo mwezi Machi hadi ya 14 ya timu 16 zinazoshiriki ligi hiyo.

No comments:

Powered by Blogger.