Ebitoke amvaa Mange Kimambi, adai siyo size yake
Msanii
Ebitoke amefunguka na kusema kuwa katika maisha yake anamchukia sana
mwanaharakati wa mitandao Mange Kimambi na kusema kuwa alimkwaza sana
kuingilia maisha yake na kusababisha mashabiki wake washindwe kumuelewa
kuhusu tuhuma za yeye kuiba mume wa Mama Ashura.
Ebitoke
amesema hayo leo Mei 9, 2018 katika kipindi cha Kikaangoni
kinachorushwa na EATV na kusema kuwa mwanadada huyo aliingia katika
anga zake na kumchefua kabisa jambo ambalio liliongeza kumchukia.
"Kwanza
yule dada Mange Kimambi mimi simpendi, sijawahi kabisaa kumkubali,
sipendi mambo yake na sipendi vimtu vinavyoongea sana, yule dada
aliingilia maisha yangu na kunichafulia mpaka kwa mashabiki zangu saizi
wengine wanashindwa kunielewa. Mange Kimambi mimi siyo size yangu
kabisaa kwanza yeye mtu mzima sasa nilishangaa kwanini yeye anaingilia
maisha yangu" alisema Ebitoke.
Mbali
na hilo Ebitoke aliweza kutoa ushauri wake kwa mwanaharakati huyo wa
mitandaoni Mange Kimambi na kusema kuwa asifanye mambo ya kufuatilia
maisha ya watu bali afanye mambo yake mengine.

No comments: