Ebitoke: Bikira yangu nilimpa Ben Pol
Msanii
wa vichekesho bongo Ebitoke, ameweka wazi kuwa ahadi aliyomuahidi kumpa
Ben Pol alishaitekeleza hivyo watu wasijiulize sana.
Akiongea
na EATV, Ebitoke amesema kuwa licha ya kwamba hivi sasa hayuko tena
kwenye mahusiano na Ben Pol, lakini yeye ndiye alikuwa mwanaume wake wa
kwanza na ndiye aliyempa zawadi ya usichana wake aliyomuahidi.
“Kama ulimuahidi mtu zawadi lazima umpe, nimeshampa Ben Pol zawadi yake”, amesema Ebitoke.
Ebitoke amesema kwamba wawili hao kwa sasa hawako pamoja lakini wanaendelea kusaidiana kwenye kazi, na sio kimapenzi tena.
Ikumbukwe
kwamba baada ya Ebitoke kukiri kuwa na hisia za kimapenzi kwa Ben Pol
aliweka wazi kuwa yeye bado ni msichana na usichana wake alitunza kwa
ajili yake, hivyo kama angekuwa naye yuko tayari kumpa.

No comments: