Header Ads

Familia ya Ferguson yatoa neno



Familia ya kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson imewashukuru mashabiki na familia nzima ya michezo duniani kwa salamu na maombi yao kufuatia upasuaji aliofanyiwa mzee Fergie.
Kijana wa Ferguson ambaye pia ni kocha wa timu ya Doncaster Rovers, Darren Ferguson, ametoa shukrani hizo akisema kama familia wanaamini kila mmoja amesaidia hali ya mzee wao kuimalika kutokana na namna walivyoguswa na kila mmoja kutoa pole.
"Kwa niaba yangu na familia yangu, napenda kuwashukuru idadi kubwa ya watu ambao wameungana nasi katika kipindi kigumu cha kuumwa kwa mzee mwanzo mpaka sasa ambapo anaendelea vizuri, msaada wao umekuwa mkubwa '', amesema.
Ferguson mwenye umri wa miaka 76 alifanyiwa upasuaji wa ubongo Jumapili iliyopita Mei 5, na kwa mujibu wa ripoti ya familia ni kwamba anaendelea vizuri akiwa katika kipindi cha mapumziko na uangalizi wa kiafya.
Mtaalam huyo wa ufundi kutoka Scotland, aliiongoza Man United kutoka mwaka 1986 hadi 2013 na kuipatia mafanikio makubwa kwenye michuano mbalimbali ya ndani na barani Ulaya kwa ujumla.

No comments:

Powered by Blogger.