Joti Atoa Ufafanuzi Kuhusu Kubomolewa kwa Nyumba Yake.
Kufuatia
nyumba yake iliyopo Kisarawe kupigwa alama ya X huku akisemekana
anatakiwa aibomoe kupisha upanuzi, Komedian maarufu nchini, Lucas
Mhavile ‘Joti’ amefungukia tukio hilo ambalo limevuta hisia kwa
mashabiki wake na Watanzania wengine waliotaka kujua undani wake.
Joti
ameema; “Wanapanua barabara huku kwetu, lakini upanuzi huo wa barabara
hauhusiani kabisa na ubomoaji wa nyumba, wengi wanajua nyumba yangu
ndiyo inabomolewa, lakini sivyo kinachobomolewa ni ukuta tu.”
Eneo
la Kisarawe na Kibada sio eneo la kwanza kwa Dar es Salaam kukukumbwa
na adha ya bomoa bomoa, kabla ya hapo maeneo ya Kimara na Kinondoni Dar
es Salaam nayo ilipita bomoa bomoa.
Nyumba
ya Joti ni miongoni mwa nyumba zaidi ya 100 zilizopigwa X maeneo ya
Kisarawe pamoja na Kibada ili kupisha upanuzi wa barabara.


No comments: