Header Ads

"Lazima tushikishwe adabu" - Lucy Mayenga




Mbunge wa viti maalum (CCM) Lucy Mayenga amefunguka na kusema kuwa Jeshi la Polisi nchini Tanzania kwa sasa linafanya kazi nzuri ambayo inaonekana na kusema kuwa kitendo wanachokifanya kuwadhibiti baadhi ya wanasiasa na viongozi ni sawa kabisa kwani wanawashikisha adabu.
Lucy Mayenga amesema hayo Mei 3, 2018 bungeni na kuwaambia viongozi wa jeshi la polisi akiwepo IGP Sirro kuwa asiwe na wasiwasi wowote kwani wanafanya mambo mazuri kwa madai kuwa wapo bungeni walizoea kutukana viongozi wa nchi na kusema maneno hovyo kwenye mikutano mbalimbali.
"Hii nchi watu walizoea kudeka, watu walikuwa wamezoea kuropoka maneno ya ajabu ajabu kila siku, watu walikuwa wamezoea kutukana kwenye mikutano hovyo hovyo lazima ifike wakati tushikishwe adabu, vyama vyote vya siasa ukiwa CCM ukiwa chama chochote lazima ifike wakati ujue kwamba nchi lazima itawalike isiwe kwamba watu wanakuwa huru kiasi mtu anaweza kuamka leo asubuhi na kufanya anachotaka kwa hiyo lazima ajue kwamba akifanya jambo lolote likiwa na adhima mbaya atashughulikiwa" alisema Lucy Mayenga
Mbali na hilo Lucy Mayenga aliwapongeza Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga na kusema hao ni watu ambao wanafanya kazi vizuri sana.

No comments:

Powered by Blogger.