Mbunge John Mnyika na Bulaya watolewa bungeni
Naibu
Spika ametoa maamuzi hayo jioni ya leo Mei 9, 2018 katika mjadala wa
bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji mwaka 2018/19 ambapo Mbunge John
Mnyika alisimama akitumia kanuni ya 69(1), kutaka kuahirishwa
kuhitimishwa kwa hoja ya wizara ya Maji na Umwagiliaji ili apewe nafasi
ya kutoa hoja yake ya kwanini bajeti ya wizara hiyo isipitishwe na
Bunge.
Mara baada ya kauli hiyo, Dk Tulia alisimama akitumia kanuni ya 69(2), kusema kama Spika atakuwa na maoni kwamba kuwasilishwa kwa hoja hiyo ni kinyume cha uendeshaji bora wa shughuli za Bunge, atakataa kuitoa ili ijadiliwe.
Hivyo kutokana na mabishano ya kinanuni hayo yaliyojiri Naibu Spika Dk Tulia Ackson aliamuru Mnyika atolewe nje kwa kutoheshimu kiti cha Spika.
Mbali na Mnyika Naibu Spika Dk. Tulia Ackson amemtoa pia ndani ya Ukumbi wa Bunge, Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya (Chadema) kwa kutoheshimu kiti cha Spika.

No comments: