Yanga yakiri kupitia magumu
Hayo
yamebainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga,
Dismas Ten leo Mei 09, 2018 Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na
waandishi wa habari kuhusiana na matayarisho yao kuelekea mtanange wao
dhidi ya Tanzania Prisons mchezo utakaochezwa katika dimba la Sokoine
jijini Mbeya.
"Zipo changamoto kadhaa tunazozipitia kama timu kwa maana ya kwamba tumekuwa na wachezaji wengi majeruhi kwa muda mrefu na mpaka sasa tunaelekea ukingoni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara wapo ambao wamesharejea katika kikosi na wengine wakiwa bado hali zao hazijaimarika sana kwa maana kwamba bado hawajawa tayari kwenye kupambana", amesema Dismas.
Yanga imekwenda Mbeya ikiwa kwenye mtego wa kutoa ubingwa kwa Simba endapo itatoa sare au kufungwa kwenye mchezo huo itakuwa imevua rasmi taji la ligi kuu baada ya kudumu nalo kwa misimu mitatu mfululizo.

No comments: