"Mfahamu majira yamebadilika" - Makonda
Makonda
ametoa kauli hiyo leo Mei 09, 2018 wakati aliposhuhudia utiaji saini wa
mikataba ya matengenezo ya barabara TARURA mkoani Dar es Salaam ambapo
inajumuisha jumla ya Makampuni manane ambayo yatakuwa na kazi ya
kukarabati barabara hizo.
"Nitoe rai kwa wakandarasi, sijawahi kuwa muoga wa kusimamia haki ya wananchi hasa walipa kodi, tunawapa dhamana hii ya kutujengea barabara kwa pesa zetu tena walipa kodi wanaonunua chumvi, mafuta ya taa, mchele wanakatwa. Ile asilimia wanayokatwa ndio inawapa nyie nafasi ya kupata ajira na kazi ya kutujengea barabara. Fanyeni kwa kuwaheshimu wananchi hawa kwa uadilifu mkubwa mtengeneze barabara nzuri",amesema Makonda.
Pamoja na hayo, Makonda ameendelea kwa kusema "ule ujanja wenu ambao mliokuwa mnaufanya mfahamu majira yamebadilika kwa hiyo niwaombe pamoja na usimamizi utakaokuwepo wa TARURA lakini na nyinyi lindeni heshima ya makampuni yenu".
Kwa upande mwingine, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema endapo watatengeneza barabara kwa kiwango kizuri basi wataendelea kupata kazi.

No comments: