Dodoma, Mwanza, Tanga, ukimwi watajwa kushamiri
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu, amesema katika mikoa
11 nchini kiwango cha maambukizi ya ukimwi inazidi kuongezeka ukiwemo
mkoa wa Dodoma, Tanga na Mwanza licha ya kiwango cha maambukizi kitaifa
kushuka kutoka asilimia 7 mwaka 2003/04,
hadi asilimia 4.7 kwa mwaka 2016/17.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa nne wa VVU na UKIMWI na miaka 30 ya mpango wa taifa wa kudhibiti Ukimwi, Waziri Ummy amesema wadau wanatakiwa kuendeleza nguvu katika maeneo ambayo maambukizi yamekuwa yakiongezeka licha ya kushuka katika ngazi ya kitaifa.
Naye Mganga mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dk. James Kiologwe, akizungumza wakati wa uzinduzi huo amesema mkoa huo unatakiwa kuongeza nguvu ya ziada kutokana na maambukizi kupanda huku wakiendelea na kampeni ya kupambana na maambukizi hayo.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya, Dk. Faustine Ndugulile, amesema mpaka sasa serikali haijapata tiba ya virusi vya ukimwi na ukimwi licha ya kuanza majaribio ya dawa kinga.

No comments: