Mpina Awaomba Wabunge Kumuunga Mkono
Kutokana
na hali hiyo Mpina pia amewataka wabunge kumuunga mkono kwa kuwa kazi
wanayopambana nayo ni nzito na inahitaji ushirikiano.
Amesema mafanikio yaliyopatikana katika operesheni hiyo ni pamoja na idadi ya samaki kuongezeka.
Akihitimisha
bajeti ya wizara yake aliyoiwasilisha bungeni jana jijini Dodoma leo,
Mpina amesema wakati wa utekelezaji wa operesheni hiyo wamefanikiwa
kukamata nyavu haramu 555431, kilo 181217, mabondo kilo 5147,pikipiki
269, na pia magari 564 yalikamatwa.
“Pamoja
na wabunge kulalamikia operesheni sangara hakuna mbunge hata mmoja
aliyewahi kunipa ushahidi wa jinsi wavuvi wanavyonyanyaswa kupitia
operesheni hiyo,” amesema Mpina.
Akithibitisha
jinsi operesheni hiyo inavyofanyika vizuri amesema wakati wa ziara ya
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa hivi karibuni wilayani Ukerewe, hakukuwa na
malalamiko yaliyotolewa na wananchi.

No comments: