Header Ads

Mugabe alitosa bunge



Aliyekuwa Rais wa Zimbabwe, Bw. Robert Mugabe kwa mara ya pili ameshindwa kutokea mbele ya kamati ya uchunguzi wa mapato ya Almasi ili kuhojiwa na kamati kuhusu madai ya upotevu wa mapato ya almasi kiasi cha Dola za Kimarekani Bilioni 15 katika kipindi cha utawala wake.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Zimbabwe Mugabe alitakiwa kwa mara ya kwanza kutokea mbele ya kamati Mei 23 , 2018 saa 3 asubuhi na kutotokea kwake kulidhaniwa kuwa ni sababu ya uzee hivyo alishindwa kufika muda wa asubuhi.
Kwa mara ya pili Mugabe alitakiwa kufika tarehe 28 Mei 2018 saa 7 mchana lakini pia ameshindwa kufika hivyo kama sheria inavyosema ataitwa mara ya 3 kabla vyombo vya dola havijapewa kazi ya kumfikisha Bungeni kwa nguvu.
"Tuliandika barua kwa Rais mstaafu kwa mara ya pili kuja lakini ameshindwa na tutaandika kwa mara ya mwisho kama inavyotakiwa na sheria, "Mbunge wa Themba Mliswa alisema.
Rais huyo mwenye umri wa miaka 94 aliyeongoza kwa muda mrefu hadi alipotolewa madarakani Novemba 2017, ametakiwa kufika Bungeni hapo Juni 11, 2018 bila kukosa.

No comments:

Powered by Blogger.