Simba na Yanga kuisaka mechi ya 4 msimu huu
Kwa msimu huu, tayari Simba na Yanga zimekutana mara tatu, wakianza Agosti 23 kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii mwaka 2017, mechi ambayo humkutanisha bingwa wa VPL na bingwa wa Kombe la FA. Katika mchezo huo Simba ilishinda kwa penalti 5-4 baada ya sare ya 0-0.
Timu hizo tena zilikutana katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Oktoba 28, 2017 na kutoka sare ya 1-1, Simba wakitangulia kwa bao la Shiza Kichuya dakika ya 57, kabla ya Obrey Chirwa kuisawazishia Yanga dakika ya 60.
Mechi ya tatu ilipigwa Aprili 29, mwaka huu ambapo bao la mlinzi, Erasto Edward Nyoni dakika ya 37 likaipa Simba SC ushindi wa 1-0, mechi zote hizo zikichezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

No comments: