Msanii wa muziki wa Bongo
fleva Nandy ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Ninogeshe'
amemshusha chini kwa nafasi moja katika mtandao wa Youtube msanii Ommy
Dimpoz ambaye naye anafanya vyema na wimbo wake wa 'Yanje'.
Nandy
sasa kwa upande wa Tanzania video yake imeshika nafasi ya kwanza katika
mtandao huo wa YouTube na kumshusha Ommy Dimpoz ambaye alikuwa ana
trend na kushika nafasi hiyo ya kwanza toka Mei 2, 2018 na sasa kushika
nafasi ya pili chini ya Nandy.
Hata hivyo mapokeo ya video hiyo ya Nandy yamekuwa ni makubwa sana
kwani video yake ndani ya siku sita toka ilipotoka Mei 3, 2018
imeshafikisha watazamaji zaidi ya Laki sita huku wengine wengi wakisema
kuwa kupitia wimbo wake huo mpya na video yake hiyo imewafanya wasahau
ujinga wake aliofanya wiki kadhaa zilizopita baada ya video yake akiwa
faragha na Bill Nas kusambaaa kwenye mitandao ya kijamii.
No comments: