Header Ads

Nimesikitishwa sana - Wenger



Kocha mkuu wa timu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema amesikitishwa sana kwa timu yake kushindwa kufuzu hatua ya fainali baada ya kukubali kufungwa na timu ya Atletico Madrid katika uwanja wa Wanda Metropolitano nchini Hispania.
Wenger amesema hayo jana Mei 03, akiongea na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mchezo huo, na kuongeza kuwa licha ya kiwango bora kilichooneshwa na wachezaji wake katika michezo yote miwili lakini wameshindwa kusonga mbele
“Najisikia vibaya kuicha timu ikiwa katika hali ya kutolewa katika mashindano kama hivi, itanichukua muda kusahau, nitaangalia cha kufanya hapo badae ila kwasasa bado sijaamua kitu chochote” amesema Wenger.
Wenger ameongeza kuwa timu ya Arsenal bado ina wachezaji wazuri ambao wataweza kutoa ushindani kwa miaka ya mbeleni na kuutaka uongozi wa timu hiyo kupanga mipango bora ya kujiandaa na msimu ujao.
Timu ya Arsenal iliondoshwa katika mashindano ya Europa baada ya kufungwa goli 1-0 na Atletico Madrid katika mchezo wa nusu fainali na kuhitimisha msimu wa mwisho kwa kocha wao Arsene Wenger ambae ataiacha klabu hiyo msimu huu baada ya kuifundisha kwa miaka 22.

No comments:

Powered by Blogger.