Niyonzima aweka rekodi ya kipekee
Niyonzima
ambaye msimu uliopita aliichezea Yanga na kutwaa ubingwa huo kwa mara
ya tatu mfululizo, msimu huu tena amefanikiwa kuchukua akiwa Simba na
kuweka rekodi hiyo ya kipekee kwenye soka la Tanzania.
Nyota huyo raia wa Rwanda hajawa na msimu mzuri sana ndani ya Simba kutokana na kusumbuliwa na jeraha la kidole kwenye mguu wa kulia, lakini sasa ameshapona baada ya kufanyiwa matibabu nchini India na huenda msimu ujao akaitumikia timu yake ipasavyo.
Kwa upande mwingine Niyonzima anaweza akaonekana kwenye mchezo wa kesho ambapo Mabingwa hao wapya watakuwa ugenini mjini Singdia kucheza na Singida United huku wakijaribu kulinda rekodi yao ya kutofungwa.
Msemaji wa Simba Haji Manara amempongeza kiungo huyo kwa kuandika ''Haruna Niyonzima anakuwa mwanadamu wa kwanza duniani kushinda ubingwa wa Tanzania mara nne mfululizo kwa vilabu viwili tofauti, rekodi hii haijawekwa na yoyote Bongo''.

No comments: