Header Ads

Rais Magufuli ahamisha bilioni 2 za UDSM



Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk. JohnMagufuli amemuagiza Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Pro, Joyce Ndalichako kuhamisha shilingi billion 2 alizopanga kupeleka chuo kikuu cha Dar es salaam kwa ajili ya ujenzi wa mabweni kuzipeleka chuo kikuu cha Sokoine cha kilimo SUA.
Rais Magufuli amefanya maamuzi hayo baada ya kubaini kuwa  kati ya wanafunzi 9,384 ni wanafunzi 3,864 pekee walio kwenye mabweni wakati akizungumza na wanafunzi pamoja na wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Sokone cha kilimo SUA baada ya kupokea malalamiko toka kwa wanafunzi wakidai wengi wao wamekua wakilazimika kulala wawili kwenye kitanda kimoja na wengine kufikia kuishi kwenye nyumba za kupanga hali inayo leta ugumu ikilinganishwa na mazingira ya Chuo.
Baada ya kupokea malalamiko hayo ameagiza kiasi cha Shilingi billion 2 zilizo pangwa kupelekwa chuo kikuu cha Dar es salaam  kwa ahadi ya Waziri wa Elimu ihamishe na kuletwa katika chuo hiki na kusisitiza umakini katika usimamizi wa fedha hizo.
Awali kabla ya kutolewa kwa agizo hilo Waziri wa Elimu Joyce Ndalichako amesema kwa mwaka huu wa fedha chuo hicho kimetengewa kiasi cha Shilingi Bilion 8 kwa ajili ya Miradi ya maendeleo.
Mtazame hapa chini Rais Magufuli

No comments:

Powered by Blogger.