Jaji Mkuu akiri kuwepo na upungufu nchini
Jaji Mkuu wa Tanzania Prof.
Ibrahim Hamis Juma amesema bado kuna upungufu mkubwa wa Majaji nchini
hali inayochangiwa na suala la maradhi mbalimbali ya kibinadamu
yanawakabali baadhi ya Majaji hao.
Prof.
Ibrahim amesema hayo leo Mei 07, 2018 Jijini Dar es Salaam, kwenye
ufunguzi wa mafunzo elekezi kwa Majaji wapya 14 Tanzania Bara na
Visiwani walioteuliwa siku za hivi karibuni na Rais Dkt. John Pombe
Magufuli ili kupata muongozo wa kuwasaidia katika shughuli zao za Ujaji.
"Kama Majaji hawatakuwa na afya imara ni wazi kwamba kesi nyingi zitakwama hivyo nawataka Majaji kuwa makini na afya zao kila siku. Juhudi za serikali za kuajiri Majaji wengi ni kusaidia kupunguza mashauri yanayokaa sana bila kushughulikiwa kwa wakati", amesema Prof. Ibrahim.
Kwa upande wake, Jaji wa Mahakama Kuu Mustapher Siyani na Jaji Aziza Idd Swed kutoka Mahakama Kuu ya Zanzibar kwa pamoja wamewataka Majaji wenzao kuacha visingizio katika utendaji kazi wao ili kurudisha imani kwa wananchi kwenye utendaji kazi wao.

No comments: