Ridhiwani anautaka Uenyekiti wa Yanga ?
“Sina lengo lolote la kutaka uongozi ndani ya Yanga labda wanachama wenyewe ndio wanatengeneza maneno hayo lakini mimi binafsi hakuna sehemu nimewahi kutamka kwasababu hata sifa tu sina mana sina kadi ya uanachama,'' amesema.
Aidha Ridhiwani ameongeza kuwa mara kadhaa watu wa Yanga wamekuwa wakiomba ushauri juu ya nini cha kufanya na amekuwa akishauri kama shabiki wa kawaida na hajawahi kuwaambia kama anahitaji kuwa kiongozi.
Yanga imeitisha mkutano mkuu wa wanachama mwezi ujao na huenda agenda kubwa ikawa ni uchaguzi kuziba nafasi ya Mwenyekiti ambayo ilikuwa inashikiliwa na Yusuf Manji kabla ya kujiuzulu mwaka jana

No comments: