Simba yaiweka Yanga kwenye mtego
Yanga
imewasili jana ikitokea nchini Algeria ilikocheza mchezo wa Kombe la
Shirikisho Afrika dhidi ya U.S.M Alger lakini imeunganisha leo kuwahi
mchezo wake huo wa kesho ambao msemaji wa Yanga Dismas Ten amesema
wanauchukulia kwa umuhimu wake.
Yanga inakwenda Mbeya ikiwa kwenye mtego wa kutoa ubingwa kwa Simba endapo itatoa sare au kufungwa kwenye mchezo huo itakuwa imevua rasmi taji la ligi kuu baada ya kudumu nalo kwa misimu mitatu mfululizo.
Simba kwasasa inahitaji alama moja tu kuweza kuwa bingwa msimu huu hivyo inaweza isisubiri mchezo wake wa jumamosi na Singida United ili ianze kusherehekea ubingwa bali inaweza kufanya hivyo kesho ednapo Yanga itakosa ushindi.
Mchezo huo wa kesho utapigwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini humo. Yanga kwasasa ina alama 48 kwenye mechi 24 huku Simba ikiwa na alama 66 kwenye mechi 27.

No comments: